Kupata Kadi Iliyopotea
Imewekwa: 12 Oct, 2022
Mpiga Kura aliyepoteza kadi ya yake ya kupigia kura anatakiwa kufuata utaratibu ufuatao ili kupata kadi nyingine:-
1. Kufika kwenye kituo ulichojiandikisha wakati wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Utaratibu huu unatumika iwapo Uboreshaji wa Daftari unaendelea.
2. Iwapo mpiga kura amepoteza kadi yake ya kupigia kura na hakuna Uboreshaji wa Daftari unaoendelea, mpiga kura anatakiwa kufika Ofisi za Tume akiwa na taarifa ya Polisi ya kupoteza kadi (Loss Report) na kujaza fomu maalum na Tume itampatia taarifa zake za mpiga kura zitakazotumika kama kitambulisho chake.