Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mzunguko wa Uchaguzi

MZUNGUKO WA UCHAGUZI TANZANIA

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 65 inaelekeza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ufanyike kila baada ya kipindi cha miaka mitano (5). Kama ilivyo kwa Nchi nyingine Duniani, katika kuendesha shughuli za Uchaguzi, Tanzania hutumia utaratibu wa mzunguko wa Uchaguzi ambao shughuli zake hugawanywa katika awamu tatu (3). Awamu hizo ni shughuli kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.

Hivyo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza mfumo wa mzunguko wa Uchaguzi kwa kufuata awamu hizo Tatu kama ifuatavyo:

(a) Kabla ya Uchaguzi

Shughuli zilizofanyika katika awamu kabla ya Uchaguzi ni pamoja na:

(i) Uandaaji wa Bajeti;

(ii) Uandikishaji wa Wapiga Kura;

(iii) Ununuzi wa Vifaa;

(iv) Uandaaji wa Kalenda na Mpango wa Utekelezaji;

(v) Marekebisho ya Sheria na Maelekezo ya Watendaji na Wadau wa Uchaguzi;

(vi) Mafunzo kwa Watendaji wa Uchaguzi;

(vii) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura; na

(b) Wakati wa Uchaguzi

Katika awamu hii, Tume ilifanya shughuli zifuatazo:

(i) Uteuzi wa Wagombea;

(ii) Uratibu wa Kampeni za Wagombea.

(iii) Utekelezaji wa Kamati za Maadili;

(iv) Usajili wa Watazamaji wa Uchaguzi.

(v) Kuchapa na kusambaza Karatasi za Kura;

(vi) Kusambaza Vifaa vya Uchaguzi;Upigaji Kura;

(vii) Kuhesabu Kura; na

(viii) Kutangaza Matokeo.

(c) Baada ya Uchaguzi

Katika awamu hii, Tume inafanya shughuli zifuatazo:

(i) Tathmini baada ya Uchaguzi Mkuu;

(ii) Kushughulikia Kesi za Uchaguzi; na

(iii) Kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu.

(iv) Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi;

(v) Kupitia na kuboresha Daftari la Wapiga Kura;

(vi) Kupitia na kuboresha Mifumo ya Uchaguzi;

(vii) Kupitia na kuboresha mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi;

(viii) Kupitia na kuboresha Muundo wa Tume;

(ix) Ukaguzi wa matumizi ya fedha na vifaa vilivyotumika katika Uchaguzi Mkuu;

(x) Kupitia Mpango Mkakati; na

(xi) Kuandaa Mpango Kazi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu unaofuata.