Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Muundo wa Taasisi

MUUNDO WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

Tume inaundwa na Wajumbe saba (7), miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano. Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Kifungu cha 5 cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Na. 2 ya Mwaka 2024..

Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka miongoni mwa Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society - TLS) na Wajumbe wengine wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa kutosha kuhusiana na kusimamia nakuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili ya kuendesha shughuli za Tume.

Tume ina jumla ya Wajumbe saba (7), kama inavyoonesha hapa chini:-

Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

Na. Jina Wadhifa

1. Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele, Mwenyekiti

2. Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk, Makamu Mweyekiti

3. Mhe. Jaji Asina Abdillah Omari, Mjumbe

4.Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri, Mjumbe

5. Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira, Mjumbe

6. Mhe. Jaji Rufaa Mwanaisha Athuman Kwariko, Mjumbe

7. Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar, Mjumbe

Wajumbe wa Tume hukaa Madarakani kwa kipindi cha miaka mitano tangu kuteuliwa kwao, lakini Rais anaweza kuwateua tena kwa kipindi kingine kadri atakavyoona inafaa. Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume husaidiwa na Sekretarieti inayoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na Katibu wa Tume. Kwa sasa Mkurugenzi wa Uchaguzi ni Kailima, R. K.

Aidha, Tume ina Idara 6, Ofisi ya Zanzibar na Vitengo 3 kama ifuatavyo:-

(i) Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi;

Bofya Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi

(ii) Idara ya Daftari na TEHAMA;

Bofya Majukumu ya Idara ya Daftari na TEHAMA

(iii) Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura;

Bofya Majukumu ya Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura

(iv) Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu;

Bofya Majukumu ya Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu

(v) Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini;

Bofya Majukumu ya Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini

(vi) Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki;

Bofya Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki

(vii) Ofisi ya Zanzibar;

Bofya Majukumu ya Ofisi ya Zanzibar

(viii) Kitengo cha Huduma za Sheria;

Bofya Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria

(ix) Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na

Bofya Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na

(x) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;

Bofya Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani