Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele amepiga kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Kisasa Jijini Dodoma, awataka wapiga kura wajitokeze kuwachagua viongozi wanaowataka

Imewekwa: 29 Oct, 2025
Mwenyekiti wa INEC, Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele amepiga kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Kisasa Jijini Dodoma, awataka wapiga kura wajitokeze kuwachagua viongozi wanaowataka

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele amejitokeza kupiga kura kwenye Kituo cha Shule ya Msingi Kisasa, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mkoani Dodoma.

Mhe. Mwambegele amewasisitiza Wapiga Kura kujitokeza kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.  Ameongeza kuwa Tume imeweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia Wapiga Kura kwa haraka. 

Watanzania kote nchini leo tarehe 29 Oktoba, 2025 wanapiga kura kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara.

Uchaguzi huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo "Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura" ambapo vituo vimefunguliwa saa 1:00 asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.