Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa) Mhe. Jacobs Mwambegele awataka wananchi wa mikoa 16 kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao

Imewekwa: 16 May, 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa) Mhe. Jacobs Mwambegele awataka wananchi wa mikoa 16 kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufani Mh. Jacobs Mwambegele  amewataka wananchi wa mikoa 16 inayojishiriki Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili na mzunguko wa pili kutumuia fursa hiyo kuboresha taarifa zao  na wengine kujiandikisha.

 

Jaji Mwambegele ameyasema hayo hiyo katika Ukumbi wa  Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani  wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji unaokwenda sambamba na Uwaekaji Wazi wa Daftari la Awali.

 

Amewasisitiza watanzania wote katika mikoa 16 inayoshiriki katika uboreshaji wa Daftari wajitokeze kwenda kuboresha taarifa zao au kujiandikisha kwa sababu baada ya siku saba kuanzia tarehe 16 hadi 22, Mei 2025, Tume haitaboresha Daftari.

 

“Wewe ambaye hutajiandikisha katika kipindi hiki cha mikoa hii 16 au wewe ambaye hutaboresha taarifa zako na kadi yako ya mpiga kura inahitaji kuboreshwa, hautaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi.” amesema Mhe. Jaji Mwambegele.

 

Ameongeza kuwa kama mpiga kura ana kadi ya mwaka 2015 au mwaka 2020 na haina tatizo ataruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi na kama mpiga kura amehama na hajaboresha taarifa zake hatashiriki kwenye uchaguzi isipokuwa uchaguzi wa Rais.

 

Aidha  Mhe. Jaji Mwambegele amewasihi watendaji hao wa uboreshaji wa Daftari ambao ni waandishi wasaidizi na waendesha kifaa cha bayometriki, kutoa huduma bora kwa wateja wao na kufuata sharia , kanuni na taratibu za uchaguzi wakati  wote wa utekelezaji wa zoezi hilo.

 

 “Mmeteuliwa kuja kushiriki tena kwa sababu ya kazi yenu nzuri, sasa nawasihi muendeleze utoaji wa huduma bora kwa wananchi kama ilivyokuwa awamu ya kwanza ya uboreshaji, hii itatufanya tufikie lengo ambalo lilikusudiwa”,  amesema Mhe. Jaji Mwambegele.

 

Wajumbe wengine wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaij Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mh. Mbaouk Salim Mbarouk, Mh. Balozi Omar Ra,madhan Mapuri, Jaji wa Mhakama Kuu Mh. Asina Omari, Mh Dkt, Zakia Mohammed Abubakar , Mh Magdalena Rwebangira na watendaji wa Tume wamehudhuria mafunzo kama hayo katika mikoa mingine.

 

Kwa uapande wake Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dr. Rogers Jacob Shemwelekwa amesema halmashauri yake imejipanga vyema kufanikisha Uboreshaji wa Daftari katika awamu hii ya pili.

 

Awamu ya Pili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unakwenda sambamba na Uwekaji wazi wa Daftari la Awali, Mikoa jiyo 16 inayoshiriki Uboreshaji  wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili na Mzunguko wa Pili ni  Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, na Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba.

 

Kauli Mbiu ya Uboreshaji  inaseama “KUJIANDIKISHA KUWAPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI  BORA’.