Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi yashiriki maonesho ya wiki ya sheria-Dodoma

Imewekwa: 12 Apr, 2024
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yashiriki maonesho ya wiki ya sheria-Dodoma

Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC inashiriki katika maonesho ya wiki ya Sheria yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.

Utaratibu huu wa kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini ni sehemu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kutoa elimu ya Mpiga Kura endelevu ambapo wadau mbalimbali wa Tume hufika katika Banda hilo na kupata elimu hiyo.

Maonesho haya ambayo huandaliwa na Mahakama ya Tanzania ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya sheria na kuanza kwa mwaka mpya wa Mahakama na mwaka huu maenesho haya yameanza tarehe 24 Januari,2024 na yanatarajia kumalizikia tarehe 30 Januari, 2024.