Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania hufanyika kila baada ya miaka mitano kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano na Makamu wa Rais, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Diwani kwa upande wa Tanzania Bara.

Ibara ya 38 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, imeweka taratibu na masharti yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeratibu na kusimamia Uchaguzi Mkuu mara Sita ambazo ni:-

  1. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 1995,
  2. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2000,
  3. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2005,
  4. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2010,
  5. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015,
  6. Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2020.