Mwenyekiti wa INEC Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele ashuhudia uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Kwahani, asema umekwenda vizuri.
08 Jun, 2024
08:00:00 - 09:00:00
Kwahani, Zanzibar
NEC
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameshuhudia wananchi wa Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi wakipiga kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kumchagua Mbunge wao na kusema umekwenda vizuri.