Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa INEC awataka makarani waongozaji wapiga kura katika Jimbo la Peramiho lililopo Songea DC, Mkoani Ruvuma kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Imewekwa: 22 Feb, 2026
Mwenyekiti wa INEC awataka makarani waongozaji wapiga kura katika Jimbo la Peramiho lililopo Songea DC, Mkoani Ruvuma kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka makarani waongozaji wapiga kura katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoani Ruvuma kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 22, 2026 wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya makarani waongozaji wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Peramiho unaotarajiwa kufanyika tarehe 26 Februari, 2026.

“Nawasihi mnapokwenda kufanya kazi yenu mkawe wakarimu na wanyenyekevu katika kutekeleza shughuli zenu... .” amesema Jaji Mwambegele.

Jaji Mwambegele amewataka washiriki hao kutoa kipaumbele kwa wapiga kura wenye mahitaji maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto wao vituoni.

“Jambo lingine nawasihi mkatende kazi yenu bila kumuogopa mtu yeyote bali mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume,” amesema Mhe. Jaji Mwambegele.