Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu avihakikishia vyama vya siasa uchaguzi huru na wa haki

Imewekwa: 12 Apr, 2024
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu avihakikishia vyama vya siasa uchaguzi huru na wa haki

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu Bw. Athumani Masasi amevihakikishia vyama vya siasa kuwa uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Bukundi utakuwa wa haki na kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya Uchaguzi.

Bw. Masasi ameyasema ofisini kwake wakati akizungumzia utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea udiwani katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Bukundi unayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatato tarehe 20 Machi, 2024.

“Na sisi tutausimamia uchaguzi kwa haki na kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo yote iliyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kwamba kila chama kinapata ridhaa kadri wananchi watakavyokuwa wamekihitaji” alisema Bw. Masasi.

Aliongeza kwa kuwaomba vyama vya siasa kuwa ni vyema wakaitumia nafasi ya kuchukua fomu za uteuzi bila ya kusubiri siku za mwisho na kwamba wasimamizi wapo tayari kutekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa tarehe ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mbali na kueleza hayo, Bw. Masasi alitoa shukrani za dhati kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mafunzo waliyoyatoa kwao wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata kwa ajili ya uchaguzi huo.

Tume ya Tiafa ya Uchaguzi ilitangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 23 za Tanzania Bara unatarajiwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2024 na fumo za uteuzi zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 27 hadi tarehe 4 Mache, 2024 ambayo itakuwa siku ya uteuzi.