Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa) Mhe. Jacobs Mwambegele na wajumbe wa Tume watembelea mafunzo ya uboreshaji wa Daftari

Imewekwa: 12 Mar, 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa) Mhe. Jacobs Mwambegele na wajumbe wa Tume watembelea mafunzo ya uboreshaji wa Daftari

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele ametembelea mafunzo ya watendaji wa uboresahji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam akiwa na Mjumbe wa Tume Mhe. Magdalena Rwebangira na kuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, ametembelea mafunzo kama katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na kuwakumbusha watendaji hao wa uboreshaji wa Daftari ngazi ya Kata kuishi kwenye viapo vyao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, alipotembelea mafunzo ya siku mbili kwa watendaji hao, katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Iddi Nyundo, uliopo kwenye ofisi za Halmashauri hiyo.

Aidha, Mhe.Asina amewataka Watendaji hao kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao ili waweze kujitokeza na kupata haki yao ya kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. 

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza Machi 17, 2025 hadi Machi 23, 2025, katika Mkoa wa Dar es Salaam.