Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari Morogoro kufanya kazi kwa weledi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amewataka washiriki wa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoa wa Morogoro kufanya kazi kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili mkoani Morogoro.
Mhe. Jaji Mwambegele ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari katika Mkoa wa Morogoro ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari katika mkoa huo.
Amesema mafunzo hayo yatahusisha pamoja na mambo mengine namna ya ujazaji wa fumo pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura uitwao Voters Registration System (VRS).
“Mafunzo haya yameandaliwa ili muweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufusaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura”, amesema Mhe. Jaji Mwambegele na kuongea kuwa:
“Nimejulishwa kuwa baadhi yenu mmeshawahi kuiriki katika katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika awamu zilizopita.”
“Kwa kutumia uzoefu mlionao na mafunzo mtakayopatiwa hii leo ninaamini mtafanya kazi zenu kwa weledi biddi na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili”
Aidha Mhe. Jaji Mwambegele amewasihi kutumia uzoefu wao walionao kuwasadia wenzao ambao hawakuwahi kushirika katika zoezi kama hilo ili kutekeleza majukumu yapo kikamilifu.
Ameongeza kuwa wakati wa uboreshahji wa Daftari maawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura.
“Jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala hao watasiadi kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutotokea kwa vuruzu zisizokuwa za lazima”, amefafanua Mhe. Jaji Mwambegele.
Mhe. Jaji Mwambegele Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa kibali kwa asasi za kiraia 157 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.
Ameongeza kuwa pia Tume imetoa kibali kwa sasi za kiraia 42 zitakazoshiriki katika uboreshaji wa Daftari ambapo kati hizo taasisi tisa ni za kimataifa na 33 ni za ndani ya nchi.
“Inasisitizwa kwa maafisa waandikishaji kuwa wanapofika katika maeneo yenu wapewe ushirikiana kwa kuwa ni wadau muhimu. Vitambulisho watakavyokuwa navyo ambavyo wamepewa na Tume ni utambulisho tosha´amesema Mhe. Jaji Mwambegele.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Balozi Omari Ramadhan Mapuri amewaasa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutekeleza majukumu waliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Mhe. Balozi Mapuri ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa daftari katika ukumbi wa MAGADU mkoani Morogoro.
Balozi Mapuri ametoa wito kwa watendaji hao kuendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote waliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao wakati wa kutekeleza zoezi lililopo mbele yao.