Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele atembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini

Imewekwa: 24 Feb, 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele atembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele leo Februari 23,2025 ametembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata katika halmashauri katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini, mkoani Morogoro na kujionea washiriki wakifanya mafunzo.

Mhe. Mwambegele  alipata fursa ya kuzungumza na washiriki hao wa mafunzo ambapo aliwasisitiza kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kujitokeza kwenye zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuanza Machi Mosi hadi Machi 07, mwaka huu Mkoani Morogoro.