Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

RC Dodoma awataka wakazi wa Dodoma kujiandikisha au kuboresha taarifa zao mapema kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Imewekwa: 26 Sep, 2024
RC Dodoma awataka wakazi wa Dodoma kujiandikisha au kuboresha taarifa zao mapema kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaasa wakazi wa Jiji la Dodoma na wilaya nyingine za mkoa huo zinazoshiriki katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kujitokeza mapema kujiandikisha au kuboresha taarifa zao na wasisubiri siku za mwisho.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo mara baada ya kuwaongoza wananchi wa Jiji la Dodoma kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura cha Shule ya Msingi Kilimani A.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga KuraMkoa wa Dodoma unahusisha Halmashauri za Wilaya ya Kongwa, Bahi na Chamwino na Jiji la Dodoma ambapo uboreshaji huo umeanza tarehe 25 Septemba hadi 1 Oktoba, 2024. 

Mbali na mkoa wa Dodoma mzunguko wa tano wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unahusisha mkoa wa Singida na Manyara katika Halmashauri za Wilaya ya Kiteto, Manyara na Mji wa Mbulu.