Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

RC Singida Mhe. Dendego awaongoza wananchi kushiriki katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Imewekwa: 26 Sep, 2024
RC Singida Mhe. Dendego awaongoza wananchi kushiriki katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Mkuu wa Mkoa wa  Singida Mhe. Halima Dendego amewaongoza wakazi wa Mkoa wa Singida kushiriki katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioanza tarehe 25 Septemba hadi 1 Oktoba, 2024 katika mkoa huo.

Mhe. Dendego ameongoza zoezi hilo kwa kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na alisingdikizwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mzunguko wa tano unashirikisha mikoa ya Singida, Dodoma katika Halmashauri za Wilaya ya Kongwa, Bahi na Chamwino na Jiji la Dodoma na  Mko wa Manyara katika Halmashauri za Wilaya ya Kiteto, Manyara na Mji wa Mbulu.