Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Taasisi na Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura na Uangalia katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chamwino na Kata 11 za Tanzania Bara

Imewekwa: 07 Oct, 2026
Taasisi na Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura na Uangalia katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chamwino na Kata 11 za Tanzania Bara

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa kibali kwa taasisi na asasi za kiraia zilizoomba kutoa elimu ya mpiga kura na kuangalizi Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Udiwani kаtika Ката 11 za Tanzania Bara

Kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na kanuni ya 22(4) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 06 Oktoba, 2026 imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na kata 11 za Tanzania Bara kwa taasisi na asasi za kiraia saba (07).

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 85(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343, kikisomwa pamoja na kanuni ya 13(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za Mwaka 2025 imetoa kibali kwa waangalizi wa uchaguzi kwa taasisi na asasi za ndani tatu (03) kwa uchaguzi mdogo tajwa.

Tume inatumia nafasi hii kuzipongeza taasisi na asasi za kiraia ambazo zimepata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura na kuwa waangalizi wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na kata 11 za Tanzania Bara. Orodha ya taasisi na asasi zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura na uangalizi wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chamwino na madiwani katika kata 11 za Tanzania.

Soma zaidi kupata Orodha ya Taasisi na Asasi zilizopata Kibali