Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Katika Jimbo la Peramiho na Udiwani Katika Kata ya Shiwinga

Imewekwa: 21 Jan, 2026
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Katika Jimbo la Peramiho na Udiwani Katika Kata ya Shiwinga

Kwa mujibu wa Taarifa ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima, Turne Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kuhusu kifo cha mbunge mmoja na diwani mteule mmoja kama ifuatavyo: 1.

Taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Peramiho, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Nafasi hiyo ilitokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo tajwa Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichotokea tarehe 11 Disemba, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 49(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024.

Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) k~husu kifo cha Ndugu Lusekelo Mwalukomo, aliyekuwa Diwani mteule wa Kata ya Shiwinga iliyopo Jimbo la Mbozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichotokea tarehe 26 Novemba, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 106(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka2024.

Aidha, kutokana na vifo hivyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 49(1)(b), 49(2), 49(4), 61(1), 68(2) na 106(2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Turne inatoa taarifa kwa umma kuhusu ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Peramiho Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma na Udiwani Kata ya Shiwinga iliyopo Jimbo la Mbozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe kama ifuatavyo:

Fomu za uteuzi kwa wagombea wa Ubunge katika Jimbo la Peramiho na Udiwani katika Kata ya Shiwinga zitatolewa kuanzia tarehe 29 Januari, 2026 hadi 04 Februari, 2026;

Uteuzi wa wagombea wa Ubunge katika Jimbo la Perarniho na Udiwani katika Kata ya Shiwinga utafanyika tarehe 04 Februari, 2026;

Kampeni za uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Peramiho na Udiwani katika Kata ya Shiwinga zitafanyika kuanzia tarehe 05 Februari, 2026 hadi 25 Februari, 2026;

na Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Perarniho na Udiwani katika Kata ya Shiwinga utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 26 Februari, 2026.

Tume inatumia nafasi hii kuvikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na Maelekezo ya Tume katika kufanikisha ratiba ya Uchaguzi husika.