Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yatangaza nafasi za kazi za watendaji wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kwahani utakaofanyika Juni, 8, 2024

Imewekwa: 03 May, 2024
Tume yatangaza nafasi za kazi za watendaji wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kwahani utakaofanyika Juni, 8, 2024

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza nafasi za kazi za watendaji wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani utakaotanyika siku ya Jumamosi tarehe 8 Juni, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Tume inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar tarehe 08 Juni, 2024.  Katika kutekeleza jukumu hilo, Tume inatangaza nafasi za kazi ili kupata Watendaji watakaosimamia zoezi hilo.  Nafasi za kazi hizo ni kama zifuatazo: -

  1. Msimamizi wa Uchaguzi (Nafasi moja)

           Majukumu

  1. Kuratibu na kusimamia shughuli za Uchaguzi katika Wilaya husika.
  2. Kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa Watendaji wa Uchaguzi walio chini yake.
  3. Kutunza vifaa vya Uchaguzi katika Wilaya husika.
  4. Kusimamia matumizi ya fedha za Uchaguzi.
  5. Kushirikiana na kushauriana na Mratibu wa Uchaguzi katika kuleta ufanisi kwenye shughuli za Uchaguzi.
  6. Kutoa taarifa ya mwenendo wa hatua za uchaguzi kwa kuzingatia maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

 

         Sifa za Msimamizi wa Uchaguzi

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe mtumishi wa Umma.
  3. Awe na Shahada au stashahada ya juu, Stashahada au Astashahada katika fani yoyote.
  4. Awe mkazi wa Wilaya husika.
  5. Awe muadilifu na mwaminifu.
  6. Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
  7. Awe na uzoefu katika masuala ya Uchaguzi/Uandikishaji wa Wapiga Kura.
  8. Ndani ya miaka mitano awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita.
  9. Awe hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa kwa kipindi cha miaka mitano.

 

  1. Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo (Nafasi mbili)

          Majukumu

  1. Kusimamia shughuli zote za Uchaguzi katika Jimbo husika.
  2. Kumsaidia Msimamizi wa Uchaguzi katika masuala yote ya Uchaguzi.

 

Sifa za Mwombaji

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe ni Mtumishi wa Umma.
  3. Awe na Shahada au Stashahada ya juu au stashahada katika fani yoyote.
  4. Awe mkazi wa Wilaya husika.
  5. Awe tayari kujituma na kuweza kufanya kazi bila ya usimamizi wa karibu.
  6. Awe na Uzoefu katika masuala ya Uchaguzi/Uandikishaji wa       Wapiga Kura.
  7. Awe muadilifu na mwaminifu.
  8. Awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai na kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita.
  9. Awe hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

Kila Mwombaji katika nafasi husika aainishe nafasi anayoiomba na aambatishe maelezo ya taarifa binafsi (CV) akiweka Jina la Taasisi anayofanyia kazi na cheo chake.  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 07 Mei, 2024 saa 9:30 Alasiri.

Barua zote zielekezwe kwa:

Mkurugenzi wa Uchaguzi,

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,

Ofisi ya Zanzibar,

Mtaa wa Maisara,

S. L. P. 4670,    

Zanzibar.

 

MUHIMU: Maombi yote yatapokelewa katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Maisara, Unguja.