Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yatoa mwaliko wa Waangalizi wa Ndani wanaotaka kuangalia Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kwahani

Imewekwa: 03 May, 2024
Tume yatoa mwaliko wa Waangalizi wa Ndani wanaotaka kuangalia Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kwahani

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa mwaliko kutoka kwa taasisi na asasi mbalimbali za ndani ya nchi ambazo zinahitaji kutazama uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kwahani utakaofanyika tarehe 8 Juni, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo la mwaliko lililosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,  Tume inatarajia kufanya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani lililopo katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar. Uchaguzi huo utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 8 Juni, 2024. 

Kwa mujibu wa kifungu cha 85(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hualika waangalizi wa uchaguzi  wanaotaka kutazama uchaguzi.

Kupitia tangazo hili, Tume inakaribisha maombi kutoka kwa taasisi na asasi mbalimbali nchini ambazo zinahitaji kutazama uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kwahani.

Taasisi na asasi zenye nia ya kuangalia uchaguzi huo ziwasilishe maombi kwa kutumia anuani (link) ifuatayo https://oms.inec.go.tz

Barua ya maombi pamoja na mambo mengine itatakiwa kuainisha mambo yafuatayo: -

  1. anuani kamili ya taasisi au asasi husika;
  2. mahali ambapo taasisi au asasi husika inafanyia kazi (Physical address);
  3. shughuli ambazo zinafanywa na taasisi au asasi husika kwa mujibu wa hati ya usajili;
  4. maeneo ambayo taasisi au asasi inapenda kwenda kuangalia uchaguzi;
  5. idadi ya watu ambao taasisi au asasi itawatumia katika zoezi hilo pamoja na majina na taarifa zao binafsi;
  6.  majina na namba za simu za viongozi wa taasisi au asasi husika kama yalivyoandikwa katika hati za usajili;
  7.  ikiwa taasisi au asasi inahusisha watendaji wa kimataifa, viongozi wawili ambao taarifa zao zitawasilishwa ni lazima wawe watanzania;
  8. kuambatisha nakala au kivuli cha hati ya usajili wa taasisi au asasi husika; na
  9.  kuambatisha nakala au kivuli cha katiba ya taasisi au asasi husika.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 7 Mei, 2024.