Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Tume yatoa ufafanuzi vigezo na masharti ya kazi za muda za watendaji wa vituo Uboreshaji wa Daftari

Imewekwa: 25 Apr, 2024
Tume yatoa ufafanuzi vigezo na masharti ya kazi za muda za watendaji wa vituo Uboreshaji wa Daftari

 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo na masharti ya kazi za muda za watendaji wa vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Katika taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima, R. K iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2024, waombaji wa kazi hizo hawatakiwa kutoa malipo yoyote.

Imefafanua taarifa hiyo kuwa mnamo tarehe 15 Aprili, 2024, tume hiyo ilitoa tangazo kupitia halmashauri zote nchini la kukaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa  vifaa vya Bayometriki kwenye vituo vya kuboresha daftari.

“Tunapenda kusisitiza kwamba barua zote za maombi ziwasilishwe kwa Maafisa Watendaji wa Kata zikiwa zimefungwa. Maafisa Watendaji wa Kata watazipokea na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika”, ilisema sehemu ya taaifa hiyo na kuongeza:

Mwombaji hatakiwa kutoa malipo yoyote”.          

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ipo kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na sehemu ya maandalizi hayo ni Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utafanyika kwa tarehe itakayotangazwa na Tume.