Makamu Mwenyekiti wa INEC atembelea na kukagua maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe
Imewekwa: 19 Feb, 2026
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo Februari 19, 2026 akiwa na Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wametembelea na kukagua maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe
Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata hiyo unatarajiwa kufanyika Siku ya Alhamisi tarehe 26 Februari Mwaka 2026.

