Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Wagombea 14 wateuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Kwahani

Imewekwa: 23 May, 2024
Wagombea 14 wateuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Kwahani

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar Bi. Safia Iddi Muhammad amefanya uteuzi wa wa wagombea kutoka vyam 14 vya siasa kuwania nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8 Juni, 2024.

Bi. Safia amefanya uteuzi huo leo tarehe 23 Mei, 2024 ikiwa ni siku ya uteuzi baada ya wagombea 14 waliochukua fomu za uteuzi kurejesha fumo hizo na kukidhi masharti ya kuteuliwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.

Wagombea walioteliwa na vyama vyao kwenye mabano ni Bi. Nuru Abdalla Shamte (DP), Bw. Bashir Yatabu Said (Demokrasia Makini), Bi. Mwanakombo Hamadi Hassan (NLD), Zainabu Maulid Abdalla (CCK), Bi. Tatu Omary Mungi (UPDP), na Bw. Khamis Yussuf Mussa (CCM).

Wengine walioteuliwa ni Bi. Jarade Ased Khamis (AAFP), Bw. Kombo Ali Juma (NRA) Bi. Shara Amran Khamis (ADC), Bi. Naima Salum Hamad (UDP), Bi. Madina Mwalim Hamad (ADA-TADEA), Bw. Amour Haji Ali (SAU), Bi. Mashavu Alawi Haji (UMD) na Bw. Abdi Khamis Ramadhan (CUF).

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo mdogo, wagombea hao wanatarajia kuanza kampeni za uchaguzi kuanzia tarehe 24 Mei, 2024 hadi tarehe 7 Juni, 2024 na siku ya uchaguzi ni tarehe 8 Juni, 2024.