Watendaji wa Uandikishaji Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia waliyojifunza
Imewekwa: 27 Jul, 2024
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira leo Julai 26,2024 wakati akifunga mafunzo kwa watendaji hao mkoani Kagera.
Aidha, amewataka kutambua kuwa jukumu la uhamasishaji wananchi linawahusu, hivyo watumie nyenzo walizonazo kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa wa kutosha ili wajitokeze kujiandikisha na kuboresha taarifa zao vituoni.
Mafunzo hayo yalihusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS).
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewajumuisha Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri.