Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Kampeni za Uchaguzi

Kwa mujibu wa Kifungu cha 46 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,Sura ya 343 na Kifungu cha 53 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Sura ya 292 kipindi cha kampeni za Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani hutangazwa na Tume. Kampeni zitaanza siku
moja baada ya siku ya Uteuzi na kumalizika siku moja kabla ya siku yaUchaguzi.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 40 ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na Kanuni ya 35 ya Kanuni za Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2020 zikisomwa pamoja na kipengele cha 2.1(c) cha Maadili ya Uchaguzi ya mwaka
2020 muda wa kuanza kampeni utakuwa saa mbili kamili (2:00)asubuhi na kumalizika saa kumi na mbili kamili (12:00) jioni.

Mratibu wa Kampeni za Uchaguzi wa Rais 
Kanuni ya 40 (1-5) na 41(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 zinaeleza kuwa; Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi wa Kiti chaRais huratibiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi atapaswa kabla ya kuanza kwa Kampeni za Uchaguzi, kuvitaka Vyama vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Rais kuwasilisha ratiba za Kampeni siku saba (7) kabla ya siku ya Uteuzi.
Ratiba za Kampeni zitaonesha Tarehe, Muda, Mkoa, Wilaya na mahali ambapo Mgombea atafanya Kampeni zake. Mkurugenzi wa Uchaguzi baada ya kupokea mapendekezo ya ratiba za Kampeni kutoka kwenye Vyama vya Siasa ataitisha mkutano kwa ajili ya kuratibu Ratiba za Kampeni. Baada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi kutayarisha Ratiba ya Kampeni iliyoratibiwa atawapatia nakala hiyo wafuatao:-
(a) Vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi wa Rais;
(b) Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa;
(c) Wakuu wa Mikoa - kwa taarifa;
(d) Wasimamizi wa Uchaguzi; na
(e) Wakuu wa Polisi wa Mikoa.