Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele aridhishwa na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Ismani na Udiwani katika kata 12 za Tanzania Bara

Imewekwa: 01 Jun, 2026
Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele aridhishwa na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Ismani na Udiwani katika kata 12 za Tanzania Bara

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amesema zoezi la kupiga Kura za Ubunge katika Jimbo la Ismani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara limekwenda vizuri huku akishudia mwitikio mkubwa wa wapiga kura walio jitokeza vituoni.

Mwenyekiti huyo wa Tume Jaji Mwambegele amesema hayo leo Juni 01,2026 akiwa katika ofisi za Kijiji Igingilanyi Wilayani Iringa mara baada ya kutembelea na kukagua zoezi la kupiga kura katika vituo vya kupigia kura vya Jimbo la Ismani.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari naye ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura vituoni kwenye uchaguzi mdogo wa Kata ya Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Naye Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira, ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura vituoni kwenye uchaguzi mdogo wa Kata ya Mzimuni, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ismani na Udiwani katika kata 12 za Tanzania Bara umefanyika leo tarehe 1 Juni, 2026.

Mbali na Ketare na Kata ya Mzimuni, kata nyingine zilizofanya uchaguzi huo ni Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru; Bwongera, Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Kibiti Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.