Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Mhe. Dkt. Zakia afungua mafunzo kwa makarani waongozaji wapiga kura Jimbo la Kwahani

Imewekwa: 04 Jun, 2024
Mhe. Dkt. Zakia afungua mafunzo kwa makarani waongozaji wapiga kura Jimbo la Kwahani

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia M. Abubakar leo tarehe 04 June, 2024 amefungua mafunzo kwa Makarani waongoza Wapiga Kura yanayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja.

Mhe.Dkt.Zakia amewataka Makarani hao kufanya kazi kwa uadilifu na weledi na katika utendaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia katiba ya nchi, Sheria za Uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume.

Kabla ya kufungua Mafunzo hayo, Makarani hao wapatao 30 walikula kiapo cha kutunza Siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Bi.Safia Iddi Muhammad.

Uchaguzi wa Jimbo la Kwahani unatarajia kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 08, June, 2024.