Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yawaasa watendaji wa Uboreshaji wa Daftari kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar kufanya kazi kwa weledi

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar kufanya kazi kwa weledi.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufani Mh. Jacobs Mwambegele ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa watendaji hao wa Magereza mafunzo ambayo yameanza leo Mkoani Dodoma sambamba na Unguja kwa Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar.
Jaji Mwambegele mewahakikishia watendaji hao kuwa Tume itawapa ujuzi wa kutosha wa nadharia na vitendo ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Akifungua mafunzo kama hayo Kisiwani Unguja, Zanzibar kwa watendaji wa Vyuo vya Mafunzo, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk ametoa wito kwa watendaji hao kuvitunza vifaa vya uboreshaji wa daftari.
Jaji Mbarouk pia amewahakikishia watedaji hao kuwa maafisa kutoka Tume watakuwepo muda wote wa zoezi na kwamba endapo watapata changamoto ya aina yoyote wasisite kuwasiliana nao.
Kwa mujibu wa ratiba zoezi hilo la Uboreshaji wa Dafatri la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika kwa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 4, 2025 ambapo wanakaohusika ni raia wa Tanzania wenye sifa ambao ni mahabusu,wafungwa na wanafunzi wa vyuo vya mafunzo walihukumiwa kifungo chini ya miezi sita.
Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msinigi wa Uchaguzi Bora.