Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

NEC Logo

Elimu ya Mpiga Kura

Elimu ya Mpiga Kura ni elimu ambayo hutolewa kwa wananchi wotekwa lengo la kuwawezesha kuelewa kuhusu Sheria, Kanuni, Taratibu za mchakato mzima wa Uchaguzi, wajibu wao na umuhimu wa kushiriki katika Uchaguzi. Vilevile ni elimu isiyokuwa na hisia, ubaguzi wala itikadi za kisiasa, kidini au kikabila.

Pamoja na Elimu ya Mpiga kura, pia kuna Taarifa kwa mpiga kura ambayo inajibu maswali ya msingi kama vile, wapi atapigia kura, lini, muda gani, atarajie nini akifika kituoni, atapata matokeo ya uchaguzi n.k. Elimu na taarifa muhimu zinapowafikia wadau na wapiga kura kwa usahihi na kwa wakati kunawafanya wajiamini na hivyo kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi hatimaye kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakaowaongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala bora nchini.

Kipimo kikubwa cha Elimu ya Mpiga Kura ni idadi ya Kura zinazoharibika (Invalid ballots), pamoja na mwitikiowa wapiga kura, kwa maana ya kuangalia, je Wapiga Kura walipata taarifa za kutosha kuhusu mchakato wa uchaguzi, ikiwemo kujua wapi na lini watapiga kura.

2.4 Umuhimu wa Elimu ya Uraia

Elimu ya Uraia inahusu haki na wajibu wa raia katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii tofauti na Elimu ya mpiga kura ambayo ni sehemu ndogo ya elimu ya uraia inayogusa nyanja ya siasa. Elimu ya uraia kwa upande wake ina sifa ya kumjengea uwezo mwananchi kujitambua na kuzijua haki zake zinazomwezesha kufanya maamuzi sahihi katikamambo yanayomzunguka. Kwa mfano, katika masuala ya uchaguzi, elimu ya uraia inamfanya mwananchi ajue wajibu wake, haki yake, nafasi yake na umuhimu wa yeye kushiriki katika michakato ya uchaguzi ikiwemo kugombea nafasi za uongozi au kushiriki kuchagua pamoja na kumuwezesha kufanya maamuzi sahihi.

Wakati Elimu ya Mpiga kura inamwezesha mwananchi kuwafahamu wagombea, kujua sifa za kuwa mpiga kura, kujua wapi, lini na muda wa kupiga kura, kujua taratibu zinazotakiwa kufuatwa awapo katika kituo cha kupiga kura, Elimu ya Uraia yenyewe inajibu swali moja la

“KWA NINI”?

⚫ Kwanini nikajiandikishe?

⚫ Kwanini nigombee nafasi?

⚫ Kwanini niende kwenye Mikutano ya Kampeni?

⚫ Kwanini nikapige Kura?

⚫ Kwanini nimpigie kura fulani? n.k

Majibu ya maswali haya ndiyo yanayoweza kuongeza ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi, ambapo kipimo kikubwa cha Elimu ya Uraia ni mwitikio wa wananchi katika michakato ya

uchaguzi ikiwemo kujitokeza siku ya kupiga Kura. Elimu ya uraia ni muhimu katika kufanikisha uchaguzi kwa kuwa ina uwezo wa kuongeza idadi ya wapiga kura wanaojitokeza siku ya uchaguzi iwapo elimu hiyo itatolewa ipasavyo.

2.5 Mamlaka ya Tume katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura

Kifungu cha 10 (1) (g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Na. 2 ya Mwaka 2024 kimeipa Tume ya Tifa ya Uchaguzi mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia Taasisi, Asasi na watu wanaotaka kutoa elimu hiyo. Kutokana na matakwa ya Sheria tajwa hapo juu, Tume hutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa Elimu hiyo.

2.6 Ushirikiano wa Tume na Asasi za Kiraia

Tume imekuwa ikishirikiana na Asasi za kiraia katika kuelimisha umma kuhusu mchakato wa Uchaguzi, kwa kutoa vibali kwa Asasi za kiraia kushiriki kutoa Elimu ya Mpiga Kura. Aidha, Tume ina utaratibu wa kuzialika Asasi zinazokusudia kutoa elimu hiyo kuwasilisha maombi na zana zao za Elimu ya Mpiga Kura ili:

(i) Kupitia na kuidhinisha zana na nyenzo zote za Elimu ya Mpiga Kura zitakazotumiwa na Asasi za kiraia na wadau wote wanaojihusisha na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura;

(ii) Kupitia na kuidhinisha mipango (program) yote iliyoainishwa na wadau wa utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura;

(iii) Kufuatilia na Kuratibu mpango (program) wa utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura ili kuhakikisha kwamba inatolewa kwa umakini, usahihi bila kupotosha Wananchi na zinawafikia walengwa wote

waliokusudiwa; na

(iv) Kufanya tathmini ya zoezi zima la utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kuona iwapo Elimu hiyo imetolewa ipasavyo na imewafikia walengwa.

2.6.1 Vigezo vinavyotumika katika kutoa vibali ni pamoja na Asasi:

(i) Kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania;

(ii) Kuwa imefanya kazi Tanzania kwa kipindi kisichopungua miezi 6 tangu kusajiliwa;

(iii) Miongoni mwa Watendaji wake wakuu, wawili wanapaswa wawe Watanzania;

(iv) Kuwa haina taarifa za kuvuruga amani au kuchochea fujo; na

(v) Kuwa tayari kujigharamia katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura.

Aidha, Asasi inapowasilisha maombi hayo inatakiwa kuambatanisha:

(i) Cheti cha Usajili,

(ii) Katiba ya Asasi,

(iii) Majina ya Viongozi wa juu wa Asasi,

(iv) Anuani kamili ya makazi (Physical Address) na namba za simu za ofisini na Viongozi,

(v) Zana za Elimu ua Mpiga Kura (Vijarida, Vipeperushi, Mabango, Vipindi viivyorekodiwa, T-shirts), na

(vi) Ratiba itakayoonyesha tarehe na mahali watakapotoa Elimu ya Mpiga Kura katika halmashauri husika.

2.7 Wadau wa Elimu ya Mpiga Kura

Tume imekuwa ikishirikiana na Wadau mbalimbali wa Uchaguzi katika kuhakikisha kila mwananchi anapata Elimu ya Mpiga Kura. Wadau hao ni pamoja na;

(i) Wapiga Kura

(ii) Vyama vya Siasa,

(iii) Taasisi za Kidini (FBOs),

(iv) Asasi za Kiraia (CSOs),

(v) Vyombo vya Habari,

(vi) Jumuiya za Wanawake,

(vii) Jumuiya za Vijana,

(viii) Jumuiya za Watu wenye Ulemavu,

(ix) Taasisi za Serikali,

(x) Asasi za Kijamii (CBOs).

(xi) Washirika wa Maendeleo, na

(xii) Taasisi za Elimu.

2.8 Ushiriki wa Makundi Maalum

Tume inatambua umuhimu wa ushiriki Makundi maalum katika Uchaguzi Mkuu, makundi hayo yanahusisha watu wenye ulemavu, wanawake na vijana. Tume pia imeangalia walengwa wengine katika jamii ambao wanahitaji mikakati maalumu ili kuwafikia kama vile watu wasiojua kusoma na kuandika. Makundi ya watu waliojitenga kutokana na shughuli za kiuchumi kama vile wavuvi, wafugaji na wawindaji.

2.8.1 Watu wenye Ulemavu

Kwa kuzingatia hali zao, watu wenye Ulemavu wamekuwa na ushiriki mdogo kwenye Uchaguzi Mkuu. Hali hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na mila potofu katika baadhi ya jamii ambazo haziwapi nafasi ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kundi hili pia linakosa nafasi ya kupata taarifa sahihi na za kutosha kuhusu michakato mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi, mfano:-

⚫ Kutokufahamu uwepo wa kifaa cha kupigia kura chenye maandishi ya nukta nundu kwenye vituo (tactile ballot folder).

⚫ Matumizi ya kituturi kwamba kinamwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

⚫ Kupewa kipaumbele wafikapo vituoni.

⚫ Kuruhusiwa kwenda na wasaidizi wao.

⚫ Haki, wajibu na umuhimu wa watu wenye ulemavu kushiriki kwenye uchaguzi.

2.8.2 Wanawake

Ushiriki wa wanawake katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa umekuwa mdogo kutokana na kuwepo kwa mila potofu katika baadhi ya jamii zetu ambazo zinamnyima mwanamke nafasi ya kujitokeza na kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo kiuchumi na kisiasa. Hali hiyo pia imefanya wanawake wasipate taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu michakato ya uchaguzi kwa mfano;

⚫ Wanawake kuwa na haki ya kujiandikisha na kupiga kura.

⚫ Kipaumbele kinatolewa kwa wajawazito na wanaonyonyesha wafikapo vituoni.

⚫ Uhuru wa kushiriki mikutano ya kampeni.

⚫ Kutoa mawazo yao na kusikilizwa.

2.8.3 Vijana

Kundi la vijana ni muhimu katika michakato ya uchaguzi kwa kuwandiko wanakopatikana wapiga kura wapya. Na kwa kuwa ushiriki wao katika masuala ya siasa hutegemea jamii inayowazunguka ni rahisi vijana kupata taarifa na elimu sahihi kuhusu michakato ya uchaguzi lakini pia ni rahisi kuwapotosha panapokuwa na nia ovu.

2.8.4 Watu wasiojua kusoma na kuandika

Kutokana na hali yao ya kutokujua kusoma na kuandika kundi hili limekuwa likikosa elimu kupitia maandiko na machapisho mbalimbali hivyo, kuwa na uhitahi wa elimu maalumu kama vile;

⚫ Elimu kwa kupitia michezo ya kuigiza.

⚫ Matamasha.

⚫ Elimu kupitia redio na runinga.

⚫ Machapisho ya picha.

⚫ Muziki wenye ujumbe maalumu.

2.8.5 Makundi Maalumu  (Makundi ya watu waliojitenga kutokana na shughuli za uvuvi, ufugaji na uwindaji)

Katika jamii ya kitanzania kumekuwepo na makundi ya wadau ambao kumekua na changamoto ya kufikia, mfano,

 Wavuvi: ni kundi ambalo hutumia muda mwingi kwenye kambi za uvuvi na kujitenga na jamii. Kundi hili hupatikana zaidi maeneo ya pwani ya Bahari ya Hindi na Maziwa yanayopatikana nchini.

Wafugaji: Kundi hili ni la wafugaji ambao huhama kutoka eneo moja kwenda jingine kutafuta malisho. Jamii hii inapatikana zaidi mikoa ya Arusha na Manyara.

Wahadzabe: Hii ni jamii ya watanzania ambayo imejitenga na kuendelea kuishi maisha yao kulingana na mila na desturi zao ambazo haziwapi nafasi kubadili mfumo wa maisha. Jamii hii inapatikana zaidi Mkoani Manyara.

Makundi haya yana uelewa mdogo kuhusu michakato ya uchaguzi kutokana na ugumu wa miundombinu ya kimawasiliano yatakayowezesha kuwafikia kwa wakati kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwahamasisha. Ni jukumu la Tume kuhakikisha makundi haya yanashiriki katika michakato ya uchaguzi.

2.9 Njia za Utoaji Elimu ya Mpiga Kura

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa ikitekeleza mkakati wa kkutoa Elimu ya Mpiga Kura endelevu kwa kutumia njia zifuatazo;

(i) Mikusanyiko rasmi ya watu: Tume inatumia maonyesho mbalimbali kama vile Sabasaba, Nanenane, Mikutano ya Serikali za Mitaa (ALAT) na wiki ya vijana kwa kutoa Elimu ya mpiga Kura ana kwa ana au kuwapatia vijitabu na vipeperushivyenye kuonyesha hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi;

(ii) Mikutano na wadau: Tume hufanya mikutano na wadau mbalimbali katika kutoa elimu. Aidha, imekuwa ikiandaa mikutano katika shule mbalimbali za sekondari kwa lengo la kuwaelimisha wapiga kura watarajiwa kuhusu shughuli za Tume na michakato ya Uchaguzi ili kuwahamasisha kushiriki katika Uchaguzi;

(iii) Vipindi vya Redio na Runinga: Tume inaandaa na kutekeleza programu ya kushiriki katika vipindi mbalimbali vya redio na runinga ili kuweza kuwaelimisha wananchi kuhusu sheria na kanuni mbalimbali za Uchaguzi.

(iv) Makala za magazeti: Tume huandaa makala zinazohusu masuala ya Uchaguzi na kuzishapisha katika magazeti mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa habari na kuelimisha umma kuhusu Sheria na taratibu za uendeshaji Uchaguzi.

(v) Mitandao ya Kijamii: Tume imekuwa ikitumia mitandao ya kijamii katika kutoa habari za kuelimisha na kuhabarisha.

(vi) Vijitabu, vijarida na vipeperushi: Tume imekuwa ikiandaa vijitabu na vijarida mbalimbali ambavyo huvigawa kwa wananchi bure.

(vii) Sanaa: Tume imekuwa ikitumia nyimbo na michezo ya kuigiza ambayo huandaliwa kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali. Nyimbo hizo na michezo hutumika katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

(viii) Gari la Matangazo: Tume hutumia gari lake la matangazo ambalo hupita katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu kama vile stendi, sokoni, minadani na shuleni ili kutoa Elimu ya Mpiga kura ana kwa ana.

2.10 Zana za Elimu ya Mpiga Kura

Katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura, Tume hutumia zana zifuatazo:

(i) Vijitabu;

(ii) Vijarida;

(iii) Vipeperushi;

(iv) Mabango; na

(v) Matangazo ya Runinga, Redio na Magazeti katika kuelimisha wananchi.

Elimu ya Mpiga Kura ni elimu ambayo hutolewa kwa wananchi wotekwa lengo la kuwawezesha kuelewa kuhusu Sheria, Kanuni, Taratibu za mchakato mzima wa Uchaguzi, wajibu wao na umuhimu wa kushiriki katika Uchaguzi. Vilevile ni elimu isiyokuwa na hisia, ubaguzi wala itikadi za kisiasa, kidini au kikabila.

Pamoja na Elimu ya Mpiga kura, pia kuna Taarifa kwa mpiga kura ambayo inajibu maswali ya msingi kama vile, wapi atapigia kura, lini, muda gani, atarajie nini akifika kituoni, atapata matokeo ya uchaguzi n.k. Elimu na taarifa muhimu zinapowafikia wadau na wapiga kura kwa usahihi na kwa wakati kunawafanya wajiamini na hivyo kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi hatimaye kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi na ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua viongozi wao watakaowaongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala bora nchini.

Kipimo kikubwa cha Elimu ya Mpiga Kura ni idadi ya Kura zinazoharibika (Invalid ballots), pamoja na mwitikiowa wapiga kura, kwa maana ya kuangalia, je Wapiga Kura walipata taarifa za kutosha kuhusu mchakato wa uchaguzi, ikiwemo kujua wapi na lini watapiga kura.

2.4 Umuhimu wa Elimu ya Uraia

Elimu ya Uraia inahusu haki na wajibu wa raia katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii tofauti na Elimu ya mpiga kura ambayo ni sehemu ndogo ya elimu ya uraia inayogusa nyanja ya siasa. Elimu ya uraia kwa upande wake ina sifa ya kumjengea uwezo mwananchi kujitambua na kuzijua haki zake zinazomwezesha kufanya maamuzi sahihi katikamambo yanayomzunguka. Kwa mfano, katika masuala ya uchaguzi, elimu ya uraia inamfanya mwananchi ajue wajibu wake, haki yake, nafasi yake na umuhimu wa yeye kushiriki katika michakato ya uchaguzi ikiwemo kugombea nafasi za uongozi au kushiriki kuchagua pamoja na kumuwezesha kufanya maamuzi sahihi.

Wakati Elimu ya Mpiga kura inamwezesha mwananchi kuwafahamu wagombea, kujua sifa za kuwa mpiga kura, kujua wapi, lini na muda wa kupiga kura, kujua taratibu zinazotakiwa kufuatwa awapo katika kituo cha kupiga kura, Elimu ya Uraia yenyewe inajibu swali moja la

“KWA NINI”?

⚫ Kwanini nikajiandikishe?

⚫ Kwanini nigombee nafasi?

⚫ Kwanini niende kwenye Mikutano ya Kampeni?

⚫ Kwanini nikapige Kura?

⚫ Kwanini nimpigie kura fulani? n.k

Majibu ya maswali haya ndiyo yanayoweza kuongeza ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uchaguzi, ambapo kipimo kikubwa cha Elimu ya Uraia ni mwitikio wa wananchi katika michakato ya

uchaguzi ikiwemo kujitokeza siku ya kupiga Kura. Elimu ya uraia ni muhimu katika kufanikisha uchaguzi kwa kuwa ina uwezo wa kuongeza idadi ya wapiga kura wanaojitokeza siku ya uchaguzi iwapo elimu hiyo itatolewa ipasavyo.

2.5 Mamlaka ya Tume katika kutoa Elimu ya Mpiga Kura

Kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kimeipa Tume ya Tifa ya Uchaguzi mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura nchi nzima, kuratibu na kusimamia Taasisi, Asasi na watu wanaotaka kutoa elimu hiyo. Kutokana na matakwa ya Sheria tajwa hapo juu, Tume hutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia zilizopata kibali cha kutoa Elimu hiyo.